Sheria Kiganjani Imesaini makubaliano ya ushirikiano na Mamlaka ya Elimu na ufundi Stadi Tanzania (VETA), Makubaliano haya yanalenga katika miradi ya kuwawezesha vijana kupata ujuzi na utaalamu wa fani mbalimbali nchini Tanzania ambapo Jumla ya vijana 13,000 wanatarajia kupokea mafunzo haya kwa kuanzia na mikoa minne ya kimkakati.
Katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa VETA CPA Antony Kasore akisaini mkabata huu pamoja na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bw.Chris Bwemo, na pia Mkurugenzi wa Mafunzo wa VETA Dr. Abdallah Ngodu na Mkurugenzi wa Teknlojia wa Sheria Kiganjani Bw. Mussa Kisena Pamoja na uongozi wa juu wa VETA. Utiaji saini huu umefanyika katika ofisi za Makao Makuu ya VETA Dodoma.Kwa maelezo zaidi tafadhali bonyeza hapa.